Sala


http://www.youtube.com/watch?v=QzcIlyzr9h8
Bild "Uetikon_Rosaire.jpg"Nakwamkia Maria,
Umejaa neema,
Bwana yu nawe,
Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria Mtakatifu
mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.

Salam Malkia / Salve Regina

Salam, Malkia!
Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam!
Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva.
Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika huku bondeni kwenye machozi.
Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho yako ya huruma,
Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
Ee mpole, Ee mwema,
Ee mpendelevu Bikira Maria.

Ishara Ya Msalaba / Sign of the Cross / Signum Crucis

Bild "Uetikon_rosenkranz.jpg"Kwa Jina la Baba
na la Mwana
na la Roho Mtakatifu.
Amina.

Imani Ya Mitume / The Apostles' Creed

Ninamwamini Mungu, Baba Mwenyezi,
Muumba wa mbingu na dunia;

Na Yesu Kristo,
Mwana wake wa pekee, Bwana wetu,
aliyetwaa mwili kwa tendo la Roho Mutakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria.
Akateswa zamani za Pontio Pilato,
akasulibiwa, akafa, akazikwa,
akashuka kuzimuni mwa wafu,
akafufuka katika wafu siku ya tatu,
akapanda mbinguni,
anakaa kwa mukono wa kuume wa Mungu,
Baba Mwenyezi,
ndipo atakuja tena kuhukumu wazima na wafu.

Ninamwamini Roho Mutakatifu,
Kanisa katolika takatifu,
ushirika wa watakatifu,
ondoleo la zambi,
ufufuko wa mwili,

na uzima wa milele.
Amina.

Baba Yetu / Our Father / Pater Noster

Baba yetu,
uliye mbinguni Jina lako litukuzwe,
ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni.
Amina.

Doxology

Kwa kuwa ufalme ni wako,
na nguvu,
na utukufu,
hata milele.

Atukuzwe Baba / Glory Be

Atukuzwe Baba,
na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo,
na sasa, na siku zote, na milele.
Amina.

Ee Yesu wangu / Oh, My Jesus (Fatima Prayer)

Ee Yesu wangu,
utusamee dhambi zetu,
utukinge na moto wa milele,
ongoza roho zote
Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi
Huruma yako.